wakufunzi wa wakulima pamoja na washauri kutoka TNS- moshi tukifuatilia kwa makini maelekezo juu ya utunzaji nauvunaji wa miche mama kutoka kwaafisa ughani wa kanda ya kaskazini, Mr. Mabagala. kwa wastani mche mama mmoja una uwezo wa kutoa machipukizi 50-150 ukipata matunzo mazuri!!!!
.
hapa machipukizi yaliyovunwa nakuchongwa vizuri yakipandwa kwenye maboksi maalumu,boksi linatakiwa kua na urefu wa 45cm ambapo 15 huwekwa kokoto, 15 huwekwa udongo wa msituni uliochanganywa na mchanga ili kurahisisha mizizi kupenya na maji kutotuama ambapo inawza kuozesha machipukizi. kwa wastani machipukizi huweza kukaakwa muda wa miezi 2.5 hadi 3 hadi kutoa miziz kutegemeana na hali ya hewa!! Ikishatoa miziz huhamishiwa kwenye viriba ambapo inaweza kukaa kwa muda wa wiki mbili hadi mwezi mmoja kabla ya kuhamishia shambani.muda wote wa kuotesha machipukizi huwa kwenye mazingira maalumu ambapo mwanga wa jua hudhibitiwa ambapo 30% ya mwanga huruhusiwa kuingia( under shade nets)
sifa kubwa ya kutumia machipukizi haya ya mbegu mpya ya kahawa tokaTaCRI ni kwamba inazaa sana kama inavyoonekana ktk picha - mshauri akikagua matunda ya kahawa katika mojawapo ya mashamba yaliyopo TaCRI- Lyamungo -Moshi
inavutia kuzitazama na kuzihgusa pia!! msahauri akikagua matunda ya kahawa -Lyamungo
wakufunzi wakishangaa jinsi kahawa zilivyozaa vizuri!! kila mtu anatamani na akaweka nia ya kuanzisha vikundi vya kuzalisha miche mama ya kahawa kwaajili ya kuzalisha miche mipya mingi kadiri iwezekanavyo katkia maeneo yetu!!
" si unaone eeh! cheki ilivyozaa halafu ina afya ajabu! inapendeza eeh!"
AHSANTE TaCRI kwa mafunzo mazuri kazi kwetu kufuata kile tulichojifunza!! matunda ndo kama unavyoyaona haihitaji maneno mengi kukushawishi!!!!! MGODI WETU NDO HUU
KILIMO KWANZA...
No comments:
Post a Comment